Tunakua Kwa Neema
Karibu kwenye tovuti rasmi ya Dayosisi ya Kaskazini Kati ya KKKT. Tuko hapa kwa ajili ya kutangaza Injili, kuimarisha imani, na kutoa huduma kwa jamii.
Huduma, Upendo, Uongozi
Karibu kwenye tovuti rasmi ya Dayosisi ya Kaskazini Kati ya KKKT. Tuko hapa kwa ajili ya kutangaza Injili, kuimarisha imani, na kutoa huduma kwa jamii.
KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Kati, inamshukuru Mungu kwamba katika hekima yake isiyopimika, na kwa njia ya Mwana wake Yesu Kristo, ametuunganisha waumini wake wote ulimwenguni kuwa wamoja.
Kwa njia hiyo, tunaweza kushirikiana pamoja na kufanikishwa katika mambo mengi. Dayosisi yetu inajihusisha na huduma mbalimbali za kijamii, kiroho, kiuchumi na kiakili kupitia idara za Misioni na Uinjilisti, Jinsia, Diakonia, Ibada na Muziki, Afya, Elimu, Mipango, Fedha na Utawala. Dayosisi ina Majimbo Saba Kanisa Kuu na Sharika 137.
Tovuti hii kwa namna iliyo bora, inaeleza mambo yote yanayofanywa na Dayosisi hii pamoja na Uongozi wake. Tunakukaribisha kutembelea Tovuti yetu.
“Tazama jinsi ilivyo vema, na kupendeza, ndugu wakae pamoja, kwa umoja”. Zab 133:1.
Wenu,
Askofu Dkt. Godson Abel Mollel
Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati.
KUHUSU SISI
Dayosisiya Kaskazini kati ya KKKT ilianza mwaka 1973, wakati huo ikijulikana kwa jina la Sinodi Mkoani Arusha, iliyoongozwa na Mchungaji Mesiaki Kilevo; akiwa kiongozi wa kwanza wa Sinodi ikiwa na Washarika 30,000, Sharika 20 na Mitaa 110.
Kiongozi wa Pili wa Sinodi alikuwa hayati Askofu Dkt Thomas Olmorijoi Laiser kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 1986.
Mwaka huo wa 1986 Sinodi ilibadilika kuwa Dayosisi Mkoani Arusha na Askofu wa kwanza akawa hayati Askofu Dkt Thomas Olmorijoi Laiser.
Mwaka 2010 Dayosisi Mkoani Arusha ilibadili jina na kuwa Dayosisi ya Kaskazini Kati, baada ya Serikali ya awamu ya tatu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kuamua kuugawa Mkoa wa Arusha na kutokeza mikoa ya Arusha na Manyara.
idara za dayosisi
Idara Ya Elimu
Idaya Ya Afya
Idara ya Miradi na Mali
Idara Ya Hazina
Menejimenti ya Dayosisi
Dkt. Godson Abel
Mollel
Askofu
Mchg. Lareton Loishiye Lukumay
Msaidizi wa Askofu
Mwl. Solomon Loshilu Sambweti
Katibu
Mkuu
Mchg. Julius Rafael
Tarakwa
Naibu Katibu Mkuu-Misioni na Uinjilisti
CPA. Mussa Abraham Massanga
Naibu Katibu Mkuu-Mipango, Fedha na Utawala.